Tuesday 18 June 2013

Mh MNYIKA ASEMA 'USHAHIDI WA VIDEO UMEONYESHA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VIMEHUSIKA NA TUKIO LA SOWETO, ARUSHA

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, Mh Mnyika ametoa kauli juu ya tukio la mlipuko wa bomu uliotokea kwenye viwanja vya Soweto, jijini Arusha. Pia amezungumzia matukio mengine.

Kuhusu tukio la mlipuko kwenye viwanja vya Soweto Arusha lililotokea Jumamosi, 15 June 2013, Mh Mnyika amedai kwamba, ushahidi wa video umeonyesha kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vimeshiriki katika 'kupanga tukio, kutekeleza tukio la mauaji, kurusha bomu, kufyatua risasi kwa bastola, kufyatua risasi kwa bunduki na vitendo vingine kwenye tukio hilo...'

Mh Mnyika amemuomba rais kuwaeleza Watanzania, 'nini amekifahamu kabla ya tukio, wakati wa tukio, na sasa, kufuatia ushahidi ambao umeonyesha wazi kwamba askari wamehusika katika tukio hilo.

Kusikiliza / kuona twanga link
http://www.youtube.com/watch?v=9Mda0plu1DM&feature=player_embedded#!

No comments:

Post a Comment