Tuesday 18 June 2013

WAOMBOLEZAJI WA CHADEMA VIWANJA VYA SOWETO JIJINI ARUSHA WATIMULIWA KWA MABOMU

CHADEMA ilipanga siku hii ya Jumanne, 18 June, kuwa ni siku maalum ya kuombeleza vifo vya watu waliopoteza maisha siku ya Jumanosi, 15 June 2013, kutokana na mlipuko wa bomu uliotokea kwenye viwanja vya Soweto jijini Arusha.

Mlipuko huo ulitokea  wakati CHEDEMA ikihitimisha kampeni za uchaguzi wa madiwani wa kata ya Kaloleni.

Maombolezo nayo yalisitishwa kwa mabomu ya machozi yaliyorushwa na polisi ili kutawanya waombolezaji walio jikusanya kwenye viwanja hivyo vya Soweto.

DSCF9335
Pichani ni sehemu ya tukio, polisi walipofanya kazi yao..



Vizuizi babararani wananchi wakionyesha hisia zao

DSC09343
Pichani: Kulia ni polisi wakilinda doria, na kushoto ni moja ya eneo linalofaniywa uchunguzi kufuatia mlipuko 15 June.

Mikusanyiko katika viwanja vya Soweto ilisitishwa ili kupisha zoezi la uchunguzi kufuatia mlipuko wa bomu siku Jumamosi, 15 June 2013. Viongozi wa CHADEMA walishauriwa kuwafahamisha wafuasi wa chama hicho sehemu tofauti ya kufanyia maombolezo.

No comments:

Post a Comment