Saturday 15 June 2013

MLIPUKO WA BOMU (AVURUGA MKUTANO WA CHADEMA VIWANJA VYA SOWETO, JIJINI ARUSHA

Mkutano hadhara wa CHADEMA kufunga kampeni za udiwani kata ya Kaloleni, uliofanyika kwenye viwanja vya Soweto, jijini Arusha umeingia dosari kufuatia mlipuko wa bomu, ambapo watu watatu wanadaniwa kupoteza maisha na wengi kujeruhiwa.

   DSC07407??????????????????????
Majeruhi baada ya mlipuko.....

Mkutano huo uliudhuriwa na viongozi wa CHADEMA wakiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Mh Freeman Mbowe na mbunge wa Arusha mjini, Mh Godbless Lema ambao awakudhurika.

           ??????????????????????
 Viongozi  wa CHADEMA juu ya lorry lililokuwa likitumika kama jukwaa

Mlipuko huo unadaiwa kutokea eneo la jukwaa ambalo viongozi CHADEMA walikuwa wakitumia lakini wakati mlipuko viongozi hao walikuwa wameshuka ili kukusanya michango toka kwa wananchi, hivyo kunusurika na mlipuko huo.

Askari wa kuzuia fujo walifika eneo la tukio na kutumia mabomu ya machozi lakini askari hao walitolewa mkuku na wananchi wenye hasira, nalo gari la wagonjwa lilivunjwa vioo na wananchi kwa kile kinachodaiwa kuchelewa kufika eneo la tukio.

Kwa picha  zaidi twanga link zifuatazo......

-- http://jamiiblog.co.tz/2013/06/15/bomu-lalipuka-arusha-kwenye-mkutano-wa-chadema-watano-waofiwa-kufa-na-wengine-70-wajeruhiwa/

-- http://arusha255.blogspot.co.uk/2013/06/breaking-news-mbowe-lema-asururika.html


Kwa video baada ya mlipuko twanga link.........

http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=hUotiwu100g#at=236 


Kwa video ya hotuba za viongozi mpaka wakati wa mlipuko twanga link ifuatayo.....

http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=rDEiY2vhFI8#at=13

No comments:

Post a Comment