Saturday 15 June 2013

LADY JAYDEE v MWANA FA, MBABE AMEPATIKANA....?

Lady Jaydee na Mwana FA na tofauti katika matamasha ya muziki waliyofanya 14/15 June 2013 baada ya kuhairishwa tarehe ya awali ya 31 May 2013 kufuatia kifo cha Albert Mangwea 29 May 2013.

Wanasema , 'Iga tembo kunya,.........................'

Dhumuni la Sherehe: Lady Jaydee alisherehekea kutimiza miaka 13 ya shughuli zake za kimuziki, uzinduzi wa album yake mpya ya 'Nothing But The Truth' na pia kusheherekea siku yake ya kuzaliwa (15 June).  Mwana FA alifanya show kwa jina 'The Finest'

Eneo la tukio: Lady Jaydee alifanyia sherehe yake nje ya eneo la mgahawa anaomiliki, Nyumbani Lounge (at zero costs) eneo ambalo lina usafiri 24hrs, Mwana FA alikodisha ukumbi wa Makumbusho ya Taifa (opposite chuo cha IFM) mbali na wananchi wa kawaida.

     
Pichani: Kushoto eneo la nje ya Nyumbani Lounge, kulia ni ukimbi wa Makumbusho

Matangazo: Lady Jaydee alitangaza kupitia East Africa Radio, Times FM nk, wakati Mwana FA alitumia zaidi Clouds FM.

Viingilio: Lady Jay Dee alitoza elfu 50 (ambazo zilinunuliwa zote) na elfu 20, wakati Mwana FA alitoza elfu 50 (inasemekana zilinunuliwa zote????)

      
Pichani: Kushoto ni washabiki wa Lady Jaydee, Nyumbani Lounge, na kulia ni washabiki wa Mwana FA ndani ya ukumbi wa Makumbusho

Support kutoka kwa wanamuziki: Lady Jaydee alisindikizwa na Mr II aka Sugu (Mh Joseph Mbilinyi), Prof Jay, Juma Nature, KR, Mkoloni, nk, wakati Mwana FA alisindikizwa na Dully Sykes, Domo Kaya, Man Dojo, Linah, Kilimanjaro Band, Ben Pol, nk.

Mchango: Ingawa Lady Jaydee akutangaza ahadi, Mwana FA aliahidi kutoa 15% ya mapato ya The Finest na kuikabidhi familia ya marehemu Albert Mangwea.

     
Pichani:kushoto ni washabiki wa Lady Jaydee wakijipanga kuingia ukumbuni, na kulia ni washabiki wa Mwana FA wakisubiri kuingia ukumbini

Lady Jaydee aliungwa mkono na idadi kubwa ya washabiki ambapo wengine walishindwa kuingia kutokana na nafasi kuwa ndogo, hivyo uenda sherehe zake zilirudisha gharama na kupata faida kuliko za Mwana FA.

Mbabe, Bint Comando, aka Team Anaconda, aka Binti Machozi.....

No comments:

Post a Comment