Saturday, 11 May 2013

RUGE vs LADY JAY DEE, RUGE AKUBALI MWITO WA NAIBU WAZIRI KUWAKUTANISHA

Mzozo wa Ruge na Mr II aka Sugu ulisuluhishwa na aliyekuwa Waziri wa Habari, Michezo, Vijana na Utamaduni, Dk Emmanuel Nchimbi.

Mzozo unaorindima kwasasa kati ya Ruge na Lady Jay Dee uenda ukapata suluhu baada ya Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mh Amos Makala kujitolea kuwakutanisha.

Kwenye toleo la mwisho Lady Jay Dee, alidai ametoa trella tu, na anagetarajia kutoa Cinema kutoa yenyewe siku yoyote kabla ya mwisho wa mwezi. Siku zilizofuata Ruge alisema yupo tayari kutatua swala hilo na Lady Jay Dee.

Ruge amedai ingawa tayari amefikisha swala hilo kwenye vyombo vya sheria na nakala kupelekwa kwa Lady Jay Dee, yupo tayari kuitikia wito wa Mh. Makala kuwakutanisha na Lady Jay Dee ili ikiwezekana suluhisho lipatikane nje mahakama.

Maneno ya Ruge yanathibitisha taarifa alizotoa Lady Jay Dee siku ya Ijumaa, 10 May 2013 akidai kwamba anatakiwa mahakamani.

Lady Jay Dee anatarajia kuzindua Album yake 31 May 2013,

Zaidi? Twanga link- http://issamichuzi.blogspot.co.uk/2013/05/niko-tayari-kuzungumza-na-lady-jay-dee.html 

No comments:

Post a Comment