Sunday 7 April 2013

CHUO CHA UFUNDI ARUSHA KUZALISHA UMEME KWA MIKOA YA ARUSHA NA KILIMANJARO !

Chuo cha ufundi Arusha kimekabidhiwa kituo cha kuzalisha umeme cha Kikuletwa kilichopo wilaya ya hai mkoani Kilimanjaro, ambacho siku zijazo kitaweza kuzalisha umeme wa kukidhi mahitaji ya umeme ya mikoa ya Arusha na Kilimanjaro na ziadi kubaki.
 
Tanesco imekabidhi kituo hicho kwa Chuo cha Ufundi Arusha. Kituo hicho cha kuzalisha umeme kwa njia ya maji kilijengwa 1930 na kilikuwa na uwezo wa kuzalisha umeme kati ya megawati moja hadi moja na nusu na kilisitisha uzalishaji umeme miaka ya themanini.
 
Chuo hicho kitafufua mashine mbili kati ya tatu zilizopo ili kuanza kuzalisha umeme utakaoingizwa kwenye gridi ya taifa kabla ya kuanza mikakati ya kuzalisha umeme wa megawati 17 kwa kutumia mitambo ya kisasa.  
 
photo(25)
Pichani: Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama (katikati) akipata melezo kutoka kwa mtaalamu wa Chuo cha Ufundi Arusha. 

Chuo hicho kitakuwa cha kwanza kumiliki kituo cha kuzalisha umeme Barani Afrika, na kutatumia kutio hicho kwa ajili ya mafunzo, kuzalisha vipuri, uzalishaji wa umeme, nk

Kituo cha umeme cha Kikuletwa kina ukubwa wa hekari 400, na kinategemea maji ya mto Kware unaoanzia Mlima Kilimanjaro na mto Mbuguni unaoanzia mlima Meru, mito hiyo upata maji mwaka mzima na uongezeka kipindi cha kiangazi.

Kujua zaidi twanga link http://jamiiblog.co.tz/2013/04/05/kikuletwa-kutosheleza-umeme-arusha-na-kilimanjaro/

No comments:

Post a Comment