Monday 8 April 2013

LADY JAY DEE NA VITA DHIDI YA MDAU WA MEDIA ANAYE MWEKEA KIWINGU

Mwanamuziki mashuhuri chini Tanzania, Lady Jay Dee (Judith Wambura) ameendeleza vita dhidi ya mtu anayemwekea kiwingu kwenye shughuli zake.

Bila ya kumtaja jina,Jide amedai kwamba kuna mdau wa media anayembania kwenye anga zake kwa muda mrefu, hata baada ya kuwa kimya kwenye shughuli za muziki, mdau huyo amekuwa akimfuatilia kwenye miradi yake mingine na kujaribu kumzibia maendeleo yake.

Inaelekea Lady Jay Dee anaendeleza yale yaliyo anzishwa na Mr II na wenzake, kwani pamoja na kutoa wimbo wake wa 'Joto hasira' aliomshirikisha Prof Jay wenye ujumbe kumuhusu mdau huyo wa media, Lady Jay Dee amekuwa akitumia vyombo mbalimbali kufafanua vita vyake.

Sehemu ya maneno kwenye wimbo wake: 'Mazao twalima wote, sahani wavuta kwako, Kama chakula tule wote, kwanini chote kije kwako, Kisa mpini umeshika wewe, Vitisho kunikama mimi'

Lady Jay Dee anatarajia kutoa album mpya mwezi May 2013, kwa jina 'Nothing But the Truth' .

Pia amesema tetesi za yeye kuanzisha kituo cha radio, Kwanza FM kilihusishwa na Siku ya wajinga duniani (April fool day), lakini atalinyia kazi wazo hilo.

Kwa mahojiano yake twanga link  http://www.youtube.com/watch?v=XE6-m_BzYko  pia twanga
 http://www.youtube.com/watch?v=ICG6RdutysU

No comments:

Post a Comment