Thursday 27 December 2012

MATOKEO YA MITIHANI YA NBAA (BODI YA UHASIBU) - NOVEMBER 2012...

Matokeo ya mitihani ya NBAA (National Board of Accountants and Auditors) iliyofanyika November 2012. Kusanya nguvu alafu twanga link kujionea, kila la kheri....

http://www.nbaa-tz.org/examinations/results/Nov_exams/Results_Summary.htm

Kwa ufupi idadi ya waliofanya mitihani Nov 2012 walikuwa 3853,ongezeko la 12.9% kulinganisha na idadi ya Nov 2011 ambayo ilikuwa 3414. Idadi kubwa ya watahiniwa walikuwa wa Module E na F, sababu ikiwa ni wanafunzi wanaojiunga kutoka vyuo vinavyo tambuliwa na NBAA.

Utafiti wa NBAA unaonyesha kwamba Pass rate ya Nov 2012 imeshuka kulinganisha na ya Nov 2011, baadhi ya sababu zilizotajwa ni: Ukosefu wa materials za kufundishia, maandalizi duni, kutokuwa na juhudi binafsi kwa wanafunzi, uelewa mdogo wa mahesabu, lugha ya kiingereza, msongamano wa wanafunzi darasani, nk.

NB: (Ni ushauri wa bure) -
Tofauti na ilivyo kwa NBAA, wale wanaosoma ACCA wanapata past papers (maswali na majibu), syllabuses, nk. bila gharama online (www.accaglobal.com). Pia materials zinapatikana kwenye mitandao mingi kama: www.opentuition.com/acca , youtube, nk.

Kama unasoma NBAA na unajua unapitia topics gani ni rahisi kupitia materials za ACCA na kupunguza tatizo (angalia links kulia kwa chini).

No comments:

Post a Comment