Saturday 5 May 2012

FAINALI KOMBE LA FA UINGEREZA - 05 MAY 2012 - CHELSEA MABINGWA

19:15 Chelsea 2-1 Liverpool

NB: Saa za Afrika Mashariki

Chelsea ni mabingwa wa kombe la FA.

Uroo wa Liverpool wa kutaka kubeba vikombe viwili msimu huu umepigwa stop, na huu uenda utakuwa ujumbe kwa Man Utd kwani wameshinda Ligi kuu misimu mingi labda ni wakati wa Man City kushinda Ligi kuu.


-----------------------------------------------------------------------------------------------------
Leo ni leo, lazima kieleweke!

Baada ya safari ndefu tamati ya Kombe la FA imefika, bingwa lazima apatikane alafu mwali (aka kombe) akabidhiwe. 

Mbali na fainali hizi, Chelsea inasubiri kucheza fainali ya Kombe la Mabingwa (UEFA) terehe 19 May, ambapo kama itashinda itakuwa na hakika ya kucheza Kombe la Mabingwa msimu ujao, endepo itamaliza Ligi Kuu ikiwa njea ya top 4.

Kombe la FA lina umuhimu wake kwenye Kombe la Europa. Mshindi wa Kombe la FA, mshindi wa Kombe la Carling, na timu itakayo maliza Ligi kuu ikiwa kwenye nafasi ya 5 zitapata ticket ya kicheza kwenye kombe la Europa.

Hivyo Chelsea inahitaji kushinda ili kupata ticket ya kucheza Kombe la Europa msimu ujao iwapo itamaliza ligi kuu ikiwa nje ya top 5.

Liverpool ilishinda kikombe cha Carling, hivyo wanayo hakika ya kucheza Kombe la Europa msimu ujao. Kuongeza kikombe cha FA ni kupunguza machungu ya kufanya vibaya kwenye Ligi Kuu msimu huu.

Nani kukabidhiwa mwali leo? B'back.....


Kwa mechi za Ligi kuu angalia habari iliyotangulia hapo chini

No comments:

Post a Comment