Tuesday 30 October 2012

MECHI ZA, 30 OCT 2012 - LEAGUE (CAPITAL ONE) CUP, UINGEREZA

Leeds Utd 3- 0 Southampton
Reading 5 - 7 Arsenal
Sunderland 0 - 1  Middlesbrough
Swindon 2 - 3 Aston Villa
Wigan 2 - 4 Bradford

Arsenal yaikwepa Hurricane Sundy, imefanikiwa kuingia robo fainali!

Kipindi cha kwanza: Reading iliwapachika Arsenal magoli bila majibu kama Hurricane Sundy, mabao yaliyopatikana dk ya 12, 18 (la kujifunga), 20 na 37! Walcot akaipatia Arsenal bao la kwanza dk 45.

Kipindi Cha pili: Arsenal ilidhamiria kuondoa aibu na kufanikiwa kupata bao dk ya 64, 89 na kwa mara nyingine Walcot akaiokoa bao la nne kwenye dk za majeruhi (dk 90), hivyo mechi kwenda Extra time aka muda wa nyongeza!

Muda wa nyongeza: Ndani ya dk 5 Chamack akaipatia Arsenal bao la 5. Baada ya mapumziko kama kawaida Arsenal wakachukua likizo na kuipa Reading mwanya wa kusawazisha na kufanya ngoma kuwa 5-5. Walcot akutulia akafunga bao la 6, Chamack naye akapigilia msumari wa mwisho na kuipa Arsenal ushindi wa 7-5.

No comments:

Post a Comment