Sunday 2 September 2012

MECHI ZA 02 SEPT 2012 - LIGI KUU YA UINGEREZA

15:30 Liverpool 0-2 Arsenal
18:00 Newcastle 1-1 Aston Villa
18:00 Southampton 2-3 Manchester Utd

NB: Saa za Afrika Mashariki

Gooners waibuka kidedea Anfield, Man Utd yaokolewa na Van Parsie! 


Van Parsie anaendelea kung'ara....

Man Utd ilianza kwa kupigwa bao dk ya 16 (Lambert), Van Parsie akasawazisha baada ya dk 8 kupita na kipindi cha kwanza kumalizika nguvu sawa. Iliwachukua Southampton dk 11 za kipindi cha pili kuwachapa Man Utd bao la lipi (Morgan Schnelderlin), lakini baada ya Van Parsie kukusa penalty alifanikiwa kuipatia bao Man Utd dk ya 87, na kuongeza la ushindi dk ya 90. 

Arsenal  nao waliibuka usingizini na kuwaliza Liverpool (a.k.a Bawa la maini) bila huruma. Magoli yote ya Arsenal yalipachikwa na wachezaji wapya msimu huu. Lukas Podolski alifunga bao la kwanza dk ya 31, naye Cazola akapachika bao la pili dk ya 69.

Inaelekea Liverpool bado wapo likizo, wanayo point 1 na wanashikilia nafasi ya 18 kati ya timu 20 

Msimamo wa top ten ulivyo (point mabanoni): 1.Chelsea(9), 2.Swansea(7), 3.West Brom(7), 4.Man City(7), 5.Man Utd(6), 6.Everton(6), 7.West Ham(6), 8.Arsenal(5), 9.Wigan(4), New Castle(4) 

Alhamis na Ijumaa: Mechi za kirafiki- Brazil v South Africa (Ijumaa 21:45), Spain v Saudi Arabia (Ijumaa 22:00).

No comments:

Post a Comment