Sunday 8 July 2012

RODGER FEDERER, SERENA WILIAMS MABINGWA WA WIMBLEDON 2012

Rodger Federer (30) ameibuka na ushindi wa 4-6, 7-5, 6-3, 6-4 dhidi ya Andy Murray (25), katika fainali tennis kwa upande wa wanaume, Wimbledon 2012.

Murray alishindwa kutamba akiwa uwanja wa nyumbani, mbele ya washabiki wake akiwemo Cameroon (Waziri Mkuu wa Uingereza), David Beckam, n.k, jambo lililochangia kutokwa na machozi na kushindwa kuongea baada ya mechi.

Federer amepata ushindi wa Wimbledon kwa mara ya saba.

Kwenye upande wa fainali za wanawake zilizofanyika Jumamosi, 07 July 2012, Serena Wiliams (30)aliibuka na ushindi wa 6-1, 5-7, 6-2 dhidi ya Agnieszka Radwanska (23)

Serena ameshinda fainali za Wimbledon kwa mara wa 5, idadi sawa na ya dada yake, Venus Williams. 

No comments:

Post a Comment