Tuesday 22 May 2012

PICHA INAYO ONYESHA UUME WA RAIS JACOB ZUMA YACHAFULIWA

Picha ya kuchora yenye kuonyesha uume wa rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ni mojawapo ya picha kwenye jumba la maonyesho (Goodman Gallery) nchini humo, na inakadiriwa kuwa na thamani ya US $14,000. 

Picha hii inaitwa 'The Spear'

Picha hii imeleta mzozo nchini humo ikidaiwa kumdhalilisha rais, ambapo ombi lilipelekwa mahakamani kupata kibali cha kuzuia picha hiyo kuonyeshwa kwenye jumba hilo.

Lakini kabla ya mahakama kutoa uamuzi, jamaa wawili (Barend la Grange na Louis Mabokela) walifanikiwa kuingia kwenye jumba hilo na kuisulubu picha hiyo kwa kuipaka rangi nyekundu na nyeusi, na baadaye wakatiwa nguvuni.

Twanga link kuona jamaa wakiisulubisha picha hii- http://www.youtube.com/watch?feature=endscreen&NR=1&v=7HHJG2fyktc

No comments:

Post a Comment