Friday 25 May 2012

KESI YA PICHA YA RAIS ZUMA IMEHAHIRISHWA

Kesi ya kupinga kuonyeshwa picha ya rais Zuma inayoitwa 'The Spear' imehahirishwa baada ya wakili wa rais huyo kuangua kilio.

Ombi hilo lilifikishwa mahakamani Alhamisi, 24 May 2012, kupinga kitendo cha jumba la Goodman Gallery kuonyesha picha inayo mdhalilisha rais (kuona picha hiyo angalia habari iliyotangulia hapo chini). Ombi hilo lisisitiza sheria ya 'kuheshimu 'utu wa mtu'.

Wakili wa rais Zuma aliangua kilio alipokuwa akielezea enzi za harakati za kuikomboa South Africa toka utawala wa kibaguzi.

Pamoja na kuunga mkono hatua za kisheria zilizochukuliwa na rais Zuma, chama tawala cha ANC kinatarajia kuifikisha mahakamani Goodmans Gallery. Wananchi wengi pia wameandamana kupinga udhalilishwaji wa rais wao.

Uongozi wa Goodman Gallery umedai unaonyesha picha hiyo kwa kuzingatia sheria ya 'Uhuru wa kujieleza' (freedom of speech).

Picha hiyo imechorwa na Brett Murray, ambaye ni mwana harakati aliyetumia sanaa yake kupinga uliokuwa utawala wa serikali ya kibaguzi.

Sheria za 'Kuheshimu utu wa mtu' na Uhuru wa Kujieleza' zina haki sawa mbele ya katiba nchini Afrika Kusini.  Nani atashinda kati ya pande hizi mbili? 

No comments:

Post a Comment