Saturday 5 May 2012

MECHI ZA 05 MAY 2012 - LIGI KUU YA UINGEREZA

14:45 Arsenal 3-3 Norwich

NB Saa za Afrika Mashariki

Ohhhh, Arsenal hatarini kutocheza Ligi ya Mabingwa (UEFA) msimu ujao!

Baada ya kushindwa kupata point zote 3, sasa hatma ya Arsenal itaamuliwa na mechi za Tottenham na Newcastle kesho!

Katika kipindi cha kwanza The Gooners a.k.a Arsenal ilipachika bao la kuongoza katika sekunde ya 6 ya dakika ya kwanza, Lakini Norwich  wakasawazisha katika dakika ya 12 na kuongeza bao la pili kwenye dakika ya 26! 

Katika kipindi cha pili dakika ya 31 Arsenal walifanikiwa kupata bao la kusawazisha, na dakika 8 baadae Van Parsie akaipatia Arsenal bao la 3, lakini Dakika 5 baadae Norwich wakaibuka usingizini na kusawazisha hivyo kufanya matokeo kuwa 3-3.

Msimamo wa ligi ulivyo (point mabanoni)-
1.Man City(83), 2.Man Utd(83), 3.Arsenal(67), 4.Tottenham(65), 5.Newcastle(65), 6.Chelsea(61), 7.Everton(52), 8.Liverpool(49), 9.Fuham(49), 10.West Brom(46, 11.Sunderland(45), 12.Swansea(44), 13.Norwich(44), 14.Stoke City(44), 15.Aston Villa(37), 16.Wigan(37), 17.QPR(34), 18.Bolton(34), 19.Blackburn(31), 20.Wolves(24)


----------------------------------------------------------------------------------------------------------
2 Games 2 gooooooo!

Ni moja kati ya mechi mbili muhimu zilizo baki, ambazo Arsenal ni lazima ishinde ili kuwa na hakika ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Kutopata point zote ni kuiweka nafasi ya 3 rehani kwa faida ya Tottenham na Newcastle ambazo zinaweza kuinyakua nafasi hiyo kama zitashinda mechi zao mbili zilizobaki. Arsenal inatofautiana na timu hizi kwa point 1.

Norwich haina wasiwasi ipo nafasi ya 14 ikiwa na point 43, inayo hakika ya kucheza ligi kuu msimu ujao hivyo matokeo ya aina yoyote hayata kuwa na hathari zozote zaidi ya kubadili nafasi yao kwenye msimamo wa ligi.

Mechi za Kesho:
Newcastle v Man City, Aston Villa v Tottenham, Bolton v West Bromwich, Fulham v Sunderland, QPR v Stoke, Wolves v Everton, Man Utd v Swansea

Kwa mechi ya fainali za FA angalia hapo juu

No comments:

Post a Comment