Wednesday 2 May 2012

MECHI ZA 02 MAY 2012 - LIGI KUU YA UINGEREZA

21:45 Chelsea 0-2 Newcastle
22:00 Bolton 1-4 Tottenham

NB: Saa za Afrika Mashariki

Chelsea hiyooo yaendelea kuzama,  yasubiri fainali za UEFA Kombe la Mabingwa kujua hatma kama itacheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao! Chelsea awata msahau Cisse aliyewaliza magoli mawii ya aina yake!

Newcastle na Tottenham watoa onyo kwa Arsenal tofauti ya point sasa imebakia 1

Msimamo wa top 10 baada ya mechi hizi (point mabanoni)-
1.Man City(83), 2.Man Utd(83), 3.Arsenal(66), 4.Tottenham(65), 5.Newcastle(65), 6.Chelsea(61), 7.Everton(52), 8.Liverpool(49), 9.Fuham(49), 10.West Brom(46


-----------------------------------------------------------------------------------------------
Washabiki wa Arsenal miguuu sawaaaaaa, macho na masikio legeeeeeza!

Habari ni kwamba, Newscastle, Tottenham, na Chelsea zipo nyuma ya Arsenal kwa tofauti ya point 4 mpaka 3. Ushindi kwa mojawapo ya timu hizi ni tishio kwa Arsenal, kwani nafasi ya 3 inayo shikiliwa na Arsenal itakuwa haikaliki!

Arsenal itaomba kwa udi na uvumba Chelsea na Newcastle zitoke sare, na Tottenham ifungwe na Bolton.

Bolton inahitaji ushindi ili kujitoa kwenye nafasi ya 18, kinyume na hapo ni kama ticket ya mwanzo wa kushuka daraja.

Msimamo wa top 10 ulivyo (point mabanoni)-
1.Man City(83), 2.Man Utd(83), 3.Arsenal(66), 4.Tottenham(62), 5.Newcastle(62), 6.Chelsea(61), 7.Everton(52), 8.Liverpool(49), 9.Fuham(49), 10.West Brom(46)

Baada ya mechi hizi, timu zote 20 zitakuwa zimebakiza mechi 2 kila moja za ili kumaliza msimu.

Jumamosi:-
Ligi kuu: Arsenal v Norwich
Fainali ya FA: Chelsea v Liverpool

No comments:

Post a Comment