Wednesday 2 May 2012

UBAGUZI WA RANGI ULIVYO NCHI ZA WENZETU

Siri ya chungu..........!

Wageni  wanapo kuja kutembelea ama kuishi nchini kwetu, tunawapokea kwa ukarimu mkubwa sababu tunajua wao ni watu wenye busara ya hali ya juu.

Lakini inakuwaje pale watu wa mataifa mengine (Afrika, Asia n.k), wanapo kwenda kuishi ama kutembelea nchi za Ulaya? Baadhi ya wakazi wa nchi hizo awafurahi kuona wageni!

Kwenye chombo cha usafiri nchini Uingereza (aka kwa Bibi), abiria amejikuta mikononi mwa Pilato (vyombo vya dola) baada ya kuwakashifu abiria wakuja (wenye asili ya Asia) kwa maneno ya kibaguzi, kwa bahati nzuri ama mbaya abiria mmoja alirekodi tukio hilo na kulirusha kwenye mtandao wa Youtube. 

Nazo mamlaka husika zikaona tukio hilo na sheria ikafuata mkondo wake baada ya mtuhumiwa kujisalimisha kituoni,  na baadaye kufikishwa kwa Pilato ambapo alikiri kosa na anasubiri hukumu yake May 26.



No comments:

Post a Comment