Saturday 19 May 2012

FAINALI ZA UEFA LIGI YA MABINGWA, 19 MAY 2012 - CHELSEA YACHUKUA UBINGWA

21:45 Bayern Munich 4-5 Chelsea

NB: Saa za Afrika Mashariki

CHELSEA MABINGWA WA UEFA CHAMPIONS LEAGUE, FINALI ZA MUNICH 2012












Baada ya dk 120 matokeo yalikuwa 1-1. Kwenye penalty Chelsea ikapata 4 na Bayern Munich 3, hivyo kufanya matokeo jumla kuwa Chelsea 5 Bayern 4!

Bayern Munich walikuwa na kila nafasi ya kushinda, kwani walipata bao la kuongoza dk ya 83 Muller, lakini Drogba akasawazisha kwa kichwa kwenye dk ya 88 kufuatia mpira wa kona. Bayern Munich tena wakapata bahati ya penalty dk 95 lakini kipa wa Chelsea, Petr Cech akaipangua.

Bayern walianza kupiga matuta na kupata penalty ya kwanza, huku penalty ya Chelsea (Mata) ikipanguliwa. Lakini Bayern Munich wakajikuta wakikosa penalty ya 4(I.Olic)  na ya 5(B.Schweinsteiger), Didier Drogba akipigilia msumari wa mwisho na kuipa Chelsea ubingwa.  

Ushindi wa Chelsea ni pigo kwa Tottenham kwani  Chelsea itashiriki Ligi ya Mabingwa msimu ujao kama bingwa mtetezi wakati Tottenham iliyomaliza nafasi ya 4 kwenye Ligi kuu ya Uingereza imesukumwa nje na itashiriki Ligi ya Europa.

Chelsea imeshinda kombe hili kwa mara ya kwanza! Hongera kwa washabiki wa Chelsea.


-----------------------------------------------------------------------------------------------------
Kweli 'hakuna marefu ..........'! Ukingo wa Ligi ya Mabingwa a.k.a Uefa Champions League ndio huu, ndani ya Allianz Arena, Munich nchini Ujerumani!

Chelsea lazima ishinde kama kweli inahitaji kushiriki ligi hii msimu ujao, hii inatokana na kumaliza msimu ikiwa nafasi ya 6 kwenye Ligi Kuu ya Uingereza, wakati ni timu 4 tu za mwanzo zinazostahili kushiriki ligi hii ya mabingwa msimu ujao.

Tottenham imemaliza msimu wa ligi Kuu ya Uingereza ikiwa kwenye nafasi ya 4, iwapo Chelsea itashinda basi itakuwa ni pigo kwa Tottenham, kwani ni Chelsea ndiyo itakayo shiriki Ligi hii ya Mabingwa msimu ujao, na Tottenham itasukumwa kucheza Ligi ya Europa!  

Bayern Munich nayo lazima ishinde sababu mechi inachezwa nyumbani, na waswahili tunasema 'Mcheza kwao..........'! Ili kuthibitisha usemi huo Bayern Munich awahitaji hadhiti bali Ushindi.

Bayern itashiriki Ligi hii ya Mabingwa msimu ujao kutokana na kumaliza Ligi Kuu ya Ujerumani a.k.a Bundesliga ikiwa kwenye nafasi ya 3, tofauti na Chelsea ambayo kama itashinda lazima ipitie mechi za mchujo ( qualifying) ili ipate tiketi ya kucheza rasmi.

Ni Bayern ama Chelsea kuchukua kombe? Ni Chelsea ama Tottenham kucheza ligi hii msimu ujao?

Kujua timu iliyopanda Ligi Kuu ya Uingereza soma habari ifuayofuatayo hapo juu!

No comments:

Post a Comment