Monday, 5 March 2012

MGOMO MWINGINE WA MADAKTARI WANUKIA

Ni count down ya mgomo mwingine wa madaktari unao tegemewa kuanza nchini.

Kama kuna maafa yaliyo sababishwa na uzembe tangu nchi kupata uhuru, ni mateso na vifo vya wagonjwa vilivyotokea wakati wa mgomo wa madaktari kati ya mwezi Feb -March mwaka huu. Hakuna aliye sahau, na juhudi za usuluhishi zinaendelea ili kutekeleza madai ya madaktari.

Kufuatia kikao cha madaktari Jumamosi, 03 March 2012, mojawapo ya madai yao, madaktari wameitaka serikali kuwang'oa madarakani waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Haji Mponda na naibu wake, Anna Nkya.

Mwisho wa utekelezaji huo ni Jumatano, 07 March 2012, saa 2 asuhubi. Kinyume na utekelezaji huo mgomo mwingine utaanza.

Je, Waziri Mponda na naibu wake,L Nkya watatumia busara na kujiuzulu ili kuokoa maisha ya wagonjwa ama watajali maslahi yao? Au Serikali itawatimua viongozi hao, ama tutegemee mgomo mwingine ?

No comments:

Post a Comment