Tuesday, 6 March 2012

MECHI ZA 06 MARCH 2012 - UEFA CHAMPIONS LEAGUE

22:45 Arsenal 3-0 AC Milan
22:45 Benfica 2-0 Zenit St Petersburg

NB: Saa za Afrika Mashariki

Mpaka kwenda mapumzikoArsenal walikuwa wakingoza 3-0, waliitaji bao 1 ngoma kuwa level (4-4), lakini bahati aikuwa yao wakashindwa kupata hata bao moja kipindi cha pili! 

AC Milan ilishinda mechi ya kwanza kwa 4-0, hivyo kwa ushindi wa Arsenal wa 3-0 unaipa AC Milan nafasi ya kusonga mbele kwa ushindi wa 4-3. Kwa matokeo Arsenal wametolewa kwenye Ligi ya Machampion wa Ulaya.

Zenit nao kama wenzao Arsenal wamefungasha virago!
...............................................................................................................................................
Mpira unadunda, chochote chaweza tokea!

Arsenal wanayo kazi ya ziada kama vile 'kupanda Mlima Kilimanjaro mpaka kileleni na kushuka kwa siku moja'! Katika mechi ya kwanza iliyochezwa terehe 15 Feb kwenye uwanja wa ugenini, Arsenal walichapwa 4-0 na AC Millan.

Kwa mtaji huo, Arsenal wanatakiwa kurudisha magoli manne, na kuongeza mengine juu bila kufungwa bao lolote, kitu ambacho ni kigumu kwani AC Milan kwa kutumia nondo zao kama  Robinho, Boateng n.k mhhhh...., na pindi AC Milan wakipata bao moja la ugenini ahhhh.....bye bye aka kwaheri Arsenal.

Zenit nao walishinda 3-2 kwenye uwanja wa nyumbani lakini magoli ya ugenini ya Benfica ni kipimo, kwani leo wanacheza uwanja wa nyumbani! Hapo Zenit wanahitaji ushindi mzuri kupata hakika ya kusonga mbele.

No comments:

Post a Comment