Sunday 5 February 2012

MECHI ZA 05 FEB 2012 - LIGI KUU YA UINGEREZA

16:30 Newcastle 2-1 Aston Villa
19:00 Chelsea 3-3 Man Utd

NB: Saa za Afrika Mashariki

Newcastle imesogea nafasi ya 5, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Arsenal baada ya sherehe ya magoli dhidi ya Blackburn jana.  Newcastle imefikisha point 42 sawa na Chelsea.
Chelsea imeambulia sare, na kuiweka nafasi ya nne hatarini! Sasa nafasi ya nne inanyemelewa na Newcastle ,Arsenal, Liverpool nk. Tottenham inayoshikilia nafasi ya nne kwa point 49 inaelekea kukosa mshindani.

Man Utd imeshindwa kuongeza pressure kwa Man City inayongoza kwa point 57, na kuikaribisha Tottenham kutoa kutafuta nafasi ya pili!.

Chelsea kweli ni Jahazi kwenye mawimbi, kufuatia kesi ya madai ya ubaguzi wa rangi inayo mkabili beki wao, John Terry dhidi ya Anton Ferdinand wa QPR, ambaye ni mdogo wa beki wa Man Utd, Rio Ferdinand. Kesi hiyo imeunguruma rasmi Jumatano wiki hii. Kibaya zaidi Ijumaa wiki hii Terry amevuliwa u captain wa timu ya taifa ya England. Leo hakuchezeshwa sababu ya mejeraha (hii labda ilikuwa janja ya nyani )

Beki ya Chelsea imeonyesha udhaifu mkubwa uliosababisha penalty mbili, na kubadili ushindi wao kuwa sare ya 3-3.

Msimamo ulivyo (top 10) :
1.Man City (57), 2.Man Utd (55), 3.Tottenham (49), 4.Chelsea (43), 5.Newcastle (42), 6.Arsenal (40), 7.Liverpool (38), 8.Sunderland (33), 9.Norwich (32), 10.Swansea (30)

Hakuna mbabe kati ya Man Utd na Chelsea!

Mechi ya kesho, 6 Feb :  Liverpool v Tottenham

No comments:

Post a Comment