Aliye nacho uongezewa, asiye nacho.............!
Waziri mkuu Mizengo Pinda amedai kwamba ongezeko la posho za wabunge kutoka 70,000 mpaka 200,000 kwa siku ni muhimu ili kuwawezesha wabunge kukabiliana na gharama za maisha kama vile mikopo nk.
Takwimu za mwisho wa mwaka 2011 zilionyesha mfumuko wa bei umepanda kwa kasi kubwa. Hii ni kudhiirisha kwamba garama za maisha zimepanda sio tu kwa wabunge bali kwa kila mwananchi. Kama wabunge wamepata ongezeko hilo kufidia gharama za maisha, kwanini walimu, madaktari na wanafunzi vyuoni hawapati ongezeko?
Posho hizo utolewa wakati wa vikao vya bunge, kwa hiyo ongezeko hilo linaonyesha wazi nia ya kuwawezesha wabunge kuvuna jasho (kodi) la wananchi mfano wa msimu wa mavuno, ili wakalipe gharama za maisha! Huu ni mwanya wa matumizi mabaya ya kodi za wavuja jasho, inahitajika kupunguza na kudhibiti idadi ya siku za vikao, sababu wabunge wengine huwa wanalala wakati wa vikao.
Waziri mkuu anatetea ongezeko la posho za wabunge, kwanini ongezeko hilo lisitumike kulipia malimbikizo ya posho za madaktari, ambao wapo kwenye mgomo kwa sasa hili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaokosa huduma sababu ya mgomo? Ni aibu, viongozi wajibu wao ni kuhakikisha huduma muhimu zinatolewa kwa wananchi lakini badala yake viongozi wetu wanaweka maslahi yao mbele.
Waziri mkuu anadai kwamba wabunge wanapata 2.3m kwa mwezi na kubakia na 1.5m baada ya makato, wanajilipia nyumba za kulala wakiwa kwenye shughuli za bunge Dodoma, na wanalipia garama za magari yao.
Ni Watanzania wangapi wenye kipato kama cha wabunge, ama wenye uwezo wa kupata mikopo ya baiskeli ama kulipia usafiri wa daladala ukiachilia mbali mikopo ya magari ya kifahari kama ya waheshimiwa wabunge?
Vyama vya wafanyakazi nchini vinahitaji miundo ya uhakika hili kufanikisha migomo na madai yao na kuwa na sauti za pamoja zinazoweza kuleta mabadiliko nchini yatakayo inua maisha ya Watanzania.
Wabunge wetu wamedhihirisha ni kiasi gani walivyo na tamaa ya kujinufaisha wenyewe, badala ya kujali maisha ya wananchi wao.
No comments:
Post a Comment