Wednesday 11 January 2012

MIRAA a.k.a MIRUNGI KUPIGWA MARUFUKU NETHERLAND

Oryaaa!

Nchi ya Holland (Netherland) ina mpango wa kupiga marufuku matumizi ya Miraa (a.k.a Mirungi a.k.a Khat) ili kudhibiti athari zake kwa jamii.

Nchi hiyo kwasasa inatumika kama kituo cha kupitishia Miraa kutoka nchi za Afrika Mashariki na baadae kusambazwa nchi nyingine za ulaya.

Sababu za kupiga marufuku ni watumiaji kutojijali wao wenyewe na familia zao. Asilimia kubwa ya watumiaji wa miraa nchini humo wanatoka Ethiopia, Somalia, Kenya na Yemen.

Miraa umfanya mtumiaji kutohisi njaa, na kuongea sana nk!

Utumiaji wa miraa kupita kiasi inaweza kusababisha- upungufu wa nguvu za uzazi, matatizo ya moyo, kukosa usingizi nk.

Na matumizi ya muda mrefu yanaweza kusababisha saratani ya mdomo na kuongeza matatizo ya akili.

Kujua zaidi twanga link - http://www.bbc.co.uk/news/world-middle-east-16508238

No comments:

Post a Comment