Thursday 29 December 2011

MZOZO KATI YA IRAN NA MAREKANI UNAELEKEA PABAYA

Wakati swala la drone ya Marekani inayoshikiliwa na Iran alijatatuliwa, Iran imetoa tishio la kuziba eneo la bahari ( Strait of Hormuz) linalotumika kupitisha gas, mafuta n.k toka nchi za Kiarabu (Iran ,Iraq, Kuwait Saudi Arabia,Qatar, UAE na Oman) kama Marekani itaweka vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran kwa kutoweka wazi mipango yake ya nuclear.

Majeshi ya Iran yameonekana yakifanya mazoezi katika eneo hilo la bahari ingawa commander wa zoezi hilo amedai ni mazoezi ya kawaida. Tishio la kuziba eneo hilo limetamkwa na baadhi ya viongozi wa Iran akiwemo makamu wa rais, aliyesema kwamba kama vikwazo vitaweka, hakuna hata tone la mafuta litapitishwa eneo hilo.( http://www.youtube.com/watch?v=eZjWzVWcJdc )



Asilimia 90 ya mafuta na bidhaa zinazotokana na mafuta upitishwa eneo hilo kuelekea Marekani, Western Europe, na Asia. Huku China ikitegemea asilimia 50% ya bidhaa hizo kuendeshea viwanda vyake.

Marekani ina vituo vya kijeshi kwenye nchi jirani na Iran. Na Iran imedai itashambulia vituo hivo ikiwemo Israel kama Marekani itaanzisha vita dhidi yake!


Marekani ilivamia Iraq mwaka 2003 kwa nia ya kujiimarisha kwenye nchi za kiarabu, juhudi ambazo zimegonga ukuta na sasa inaondoa majeshi yake toka Iraq. Pia  inaelekea kupoteza washirika ikiwemo Afganstan, Misri, Syria nchi ambazo zinaimarisha mahusiano yao na Iran kwasasa. ( http://www.youtube.com/watch?v=qfuK1FiVvko )

Kama Iran itafunga eneo hilo, mauzo ya mafuta toka nchi za eneo hilo ikiwemo Iran yataathirika, lakini Iran inafanya mipango kuongeza mauzo yake kwa nchi za China na Russia kuepuka hasara hiyo.


Marekani ikiweka vikwazo dhidi ya Iran, bei ya mafuta katika soko la dunia itapanda na kuathiri uchumi wa dunia, ingawa Saudi Arabia inajiandaa kuongeza uzalishaji kufidia upungufu katika soko la dunia!

Nini kinafuata! Vita ama kupanda kwa bei ya mafuta? Na swala la drone ya Merekani litaishia wapi? Ama Iran itaweka wazi mipango yake ya nuclear kwa UN ili kuepuka vikwazo?

No comments:

Post a Comment