Wanasema ukimuamsha aliye lala..............!
Kinyume na utabiri wa wengi , Amir Khan (UK) amejikuta akipoteza mpambano dhidi ya Peterson (USA) iliyochangiwa na kukatwa point mbili (aka point deduction)
Kwa ushindi huo (113-112, 113-112, 111-114) Peterson amenyakua mikanda miwili ya IBF na WBA iliyokuwa ikishikiliwa na Amir Khan kwenye ngazi hiyo ya light-welterweight.
Kwa upande mwingine ndoto za Amir za kutaka kuunganisha mikanda yote kwenye ngazi ya light-welterweight ikiwemo ya WBO na WBC imeota majani kwa muda. Pia mbio zake za kutaka kupanda ngazi ya Welterweight ili kupambana na wababe walioshindikana Manny Pacquiao (WBO) na Floyd Mayweather (WBC) zimegota ukuta kwa muda.
Amir alimpa Peterson nafasi ya kupigana naye baada ya juhudi za muda mrefu za kutaka kupambana na Tim Bradley anayeshikilia mikanda ya WBC na WBO ya light-welterweight kushindikana.
Amir amelaumu upendeleo aliopata Peterson toka kwa msimamizi wa pambano hilo, hata hivyo Peterson amekubali kumpa Amir nafasi ya marudiano.
Angalia yaliyojiri kwenye mpambano ....... http://www.youtube.com/watch?v=Aaz3hqYDkDo
Lini marudiano na nani atashinda? Tusubiri...
No comments:
Post a Comment