Tuesday 27 December 2011

HARAKATI ZA CHINA KUWA NA SATELLITE

China sio tu inaleta ushindani kwa mataifa makubwa katika uzalishaji wa bidhaa ama kibiashara duniani, bali hata katika harakati za kuwa na satellites angani!

Tumezoea kuona bidhaa za China kila kona, hata wafanya biashara wa Kariakoo walitoa lawama kibao kuhusu wafanya biashara toka China kuchukua biashara zao, sijui harakati zile zilifikia wapi.

Inasemekana Satellites za China (Beidou) zipatazo kumi, zimeanza kufanya kazi na inatarajia kuwa na jumla ya satellites 35 angani ifikapo mwaka 2020, ambazo zitaweza kutumika katika mawasiliano duniani kote. Huu utakuwa ni ushindani dhidi ya Marekani (GPS-Global positioning System), ambayo pia inapata ushindani mwingine kutoka Russia (GLONASS) na baadae (2019) kutoka European Union (Galileo)


Wachunguzi wa mambo wanadai kwamba uenda China imekusudia kuwa na Satellites zake badala ya kutegemea mawasiliano ya Satellites za Marekani ambazo zinaweza kuzimwa pindi China itakapokuwa kwenye ya harakati za kivita dhidi ya washirika wa Marekani.

kujua zaidi twanga link-  http://www.bbc.co.uk/news/technology-16337648

No comments:

Post a Comment