Friday 2 September 2011

UGANDA INAFUATA BAADA YA LIBYA?

Upepo wa mabadiliko umepita Tunisa, Egypt, na Libya na sasa wanaharakati nchini Uganda wanadai ni wakati wao kufanya mabadiliko.

Activists For Change nchini Uganda wameitisha maandamano siku ya ijumaa kusherehekea mabadiliko yaliyotokea kaskazini mwa bala la Afrika. Kwenye vipeperushi (flayers) vya kuhamasisha maandamano hayo kuna picha za viongozi wa Tunisia, Egypt ,Libya na Uganda. Cha kushangaza ni kwamba Picha zote zimewekwa alama za X kuashiria viongozi hao wameshaondolewa , isipokuwa ya kiongozi wa Uganda kwamba inafuata kwenye mabadiliko.

Polisi wamesema eneo la kufanyia mkutano huo alijakamilika na hivyo maandamano hayo hayajaruhusiwa.

Je mabadiliko yataikumba Uganda? Je maandamano hayo yatafanyika na nini kitatokea?

No comments:

Post a Comment