Report ya CAG iliyokuwa ikichunguza tuhuma dhidi ya Jairo imetoka, kulingana na mtazamo wa David Jairo alithibitisha mbele ya waandishi wa habari kwamba Jairo hana hatia na aliamuru arudi kazini kufuatia likizo aliyokuwa amepewa ili kuruhusu uchunguzi kufanyika.
Luhajo amethibitisha idara kuchangia garama za budget ni utaratibu wa kawaida na huwa linafanyika, na alitoa onyo kwa aliyetoa siri hizo nje ya wizara kuchunguzwa na kuadhibiwa!
for more-
http://mwananchi.co.tz/component/content/article/37-tanzania-top-news-story/14798-ikulu-yamsafisha-jairo.html
-Report yenyewe( edited video) - http://www.youtube.com/watch?v=dKm0M3iWzsw
Jana ilikuwa shamra shamra wizara ya Nishati na Madini kwani wafanyakazi walimpokea Jairo kwa furaha aliporudi kazini.
Luhajo alisahau kwamba mjadala ulizuka bungeni na ndipo bunge lilipo amua uchunguzi ufanywe, na ndipo Jairo alilazimishwa kwenda likizo ili uchunguzi ufanyike. Kwa taratibu report hiyo ilitakiwa kurudishwa bungeni ili wabunge waamue nini kifuate baada ya hapo, kwani report yenyewe imethibitisha michango ya fedha ilifanywa na idara husika ,ingawa siyo kwa kiasi kilichotajwa kwenye tuhuma, na kwamba hakuna hongo iliyotolewa kwa wabunge ili Budget ipitishwe.
Pamoja na hayo uamuzi ulifikiwa na wabunge kufuatia hoja ya Mh. Zito kabwe kwamba taratibu zilikiukwa na wametaka tume maalumu iundwe kuchunguza upya ikiwemo utaratibu aliochukua Luhajo.
Swali ni kwamba je utaratibu wa kukusanya michango kutoka idara za wizara unafanyika na wizara ngapi? Kama unafanyika je ni halali wakati wizara zinapewa fungu serikalini kwa bunge kupitisha budget kila mwaka wa fedha!
Na kama utaratibu huu unafanyika kwanini wananchi ama walipa kodi tusifahamishwe,kwanini iwe siri?
Kuna haja ya serikali kuwa na transparency kwenye shughuli zake haswa zile zinazohusu matumizi ya fedha za wananchi, kwani inaonyesha viongozi waliopo madarakani wanajisahau kwamba wao ni watumishi kwa walipa kodi na sio vinginevyo.
Hatua aliyochukua Luhajo ni kinyume na matarajio ya wabunge ,waziri mkuu na wananchi kwa ujumla, Jairo uenda hana hatia lakini inaonyesha jinsi gani taratibu nyingi zinazofanywa mawizarani kwa siri na kinyume na matarajio ya walipa kodi
No comments:
Post a Comment