Sunday 9 June 2013

MECHI YA TAIFA STARS v MOROCCO, 08 JUNE 2013

Morocco imeinyuka Taifa Stars 2-1, katika mechi za kuwania kufuzu kucheza kombe la dunia Brazil 2014, iliyofanyika Marrakesh.

Mabao ya Morocco yalipatikana dk ya 37 na 50, na Taifa Stars ilipata bao la kushtukiza dk 61.

morocco a7427

Kufungwa mechi hii ni mlolongo wa matukio iliyopitia Taifa Stars, ambayo ililazimika kutumia nguvu (aka kuruka geti) kuingia kiwanjani hapo ili kufanya mazoezi baada ya kuzuliwa na walinzi. Taifa Stars ilikaribishwa kwa chakula Ikulu ili kuwapa motisha kupata ushindi dhidi ya Morocco.

Morocco imepunguza machungu ya mechi ya kwanza iliyochezwa Dar es Salaam 24 March 2013, ambapo Taifa Stars ilishinda 3-1.

Taifa Stars imebaki katika nafasi ya pili. Msimamo wa Kundi C ulivyo point mabanoni: 1.Ivory Coast (10), 2.Tanzania (6), 3.Morocco (5), 4.Gambia (1)

Mechi za Kundi C zinazofuata , 16/ 15 June: Taifa Stars v Ivory Coast, Morocco v Gambia

No comments:

Post a Comment