Sunday 5 May 2013

MLIPUKO KATIKA KANISA KATOLIKI LA St JOSEPH, OLASITI MKOANI ARUSHA

Mtu mmoja amepoteza maisha na wengine kujeruhiwa mida ya saa nne asubuhi kufuatia mlipuko unaodhaniwa ulisababishwa na bomu wakati uzinduzi wa Kanisa Katoliki la St Joseph, Parokia ya Olasiti mkoani Arusha.

 DSCN2227DSCN2236
 Eneo ambalo kilirushwa na kudondokea kitu kinacho dhaniwa kuwa ni bomu

Balozi wa Vatican nchini na ujumbe wake walioudhuria uzinduzi na hawakupata madhara yoyote. Balozi huyo alikuwa katika hatua za kukata utepe mbele ya kanisa hilo  kuhashiria ufunguzi wa kanisa hilo ndipo mlipuko huo ulipotokea.


 DSCN2226
Pichani juu ni eneo la mbele la kanisa  hilo na kushoto ni Balozi huyo na mapadri katika hatua za mwisho muda mfupi kabla ya mlipuko.
 
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas amethibitisha kuwa mtu mmoja amepoteza maisha na watu wengine wapatao 30 kujeruhiwa. Pia Kamanda huyo amethibitisha kukamatwa kwa mtu mmoja.

No comments:

Post a Comment