Wednesday 13 March 2013

PAPA KUPATIKANA LEO, 13 MARCH 2013?

Jana, 12 March 2013 Vatican City moshi mweusi ulifuka kuonyesha ishara kwamba Makardinali walishindwa kupata Papa mpya wa Kanisa Katoliki. Zoezi hilo linaendelea leo, asipopatikana zoezi litaendelea kesho.

 
Jumla ya Makardinali 115 kutoka nchi 48 wamekutana makao makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican City na kujifungia ndani ya Sistine Chapel ambapo upigaji kura unafanyika. Ili kuchaguliwa Papa lazima apate angalau 2/3 ya idadi ya kura zote, ama angalau kura 77 ya jumla ya kura zote.

Kufuka moshi mweupe ni ishiria kwamba Papa amepatikana, moshi mweusi ni ishara kwamba ajapatikana.

No comments:

Post a Comment