Wednesday 13 March 2013

KANISA KATOLIKI LIMEPATA PAPA MPYA, NI PAPA FRANCIS I

Kardinali Jorge Mario Borgoglio wa Argentina amechaguliwa  kuwa Papa mpya wa Kanisa Katoliki. Ni Papa wa 266 na ataitwa Papa Francis I.

Saa 22:12 kwa masaa ya Afrika Mashariki, jina la Papa lilitangazwa mbele ya umati wa watu walio kusanyika St Peter's Square, na baadae Papa Francis alitokeza na kuongea.

Papa Francis I akipungia umati wa watu St Peters Square 

Saa 21:06 kwa zaa za Afrika Mashariki moshi mweupe ulifuka na kengele kupigwa kuashiria kupatikana Papa mpya.

Moshi mweupe kuashiria kupatikana wa Papa mpya

Wazazi wa Papa Francis I ni Waitalia walioamia Argentina alikozaliwa na kuishi Papa Francis.

Papa Francis I amechaguliwa baada ya kustaafu Papa Benedict XVI terehe 28 February 2013.

No comments:

Post a Comment