Monday 11 February 2013

WABUNGE WA UPINZANI WAPOKEWA DAR, UONEVU WA SPIKA NA NAIBU WAFIKISHWA KWA WANANCHI

Jumapili ya 10 February 2013, Wabunge wa upinzani nchini walipokewa mjini Dar es salaam kama ishara ya kuwapongeza kwa mshikamano walioonyesha dhidi ya uonevu naofanywa Spika wa bunge Anna Makinda na naibu wake, Ndugai kwa wabunge wa vyama vya upinzani.
 
Mapokezi hayo yalifuatiwa na maandamano kuelekea Temeke kwa ajili ya mkutano kama mwanzo wa juhudi za kulaani uonevu unaofanywa na Spika wa Bunge na naibu wake. 
 
Katibu Mkuu wa Chedema, Dk Slaa akiwakilisha mashitaka kwa Wananchi
 
 
Makamanda wa Chadema wakiandamana kuelekea Temeke
 
Katibu wa Chama cha AFP aliunga mkono mkutano huo
 
Inatarajiwa wabunge kugawanyika na kuelekea katika kanda kumi kuendelea na juhudi za kufikisha malalamiko hayo kwa wananchi. (www.chademablog.blogspot.com)
 

No comments:

Post a Comment