Thursday, 7 February 2013

SLAA ATOA MSIMAMO WA CHADEMA KUHUSU UONEVU UNAOFANYWA NA SPIKA, ANNA MAKINDA

Ni 'Mwaka wa Nguvu ya Umma' , wabunge wa CHADEMA awatagoma kwa kutoka nje ya bunge tu, bali watatumia mbinu tofauti.

Katibu mkuu wa CHADEMA, Dk.W Slaa ametoa msimamo wa chama hicho kuhusu unyanyasaji unaofanya na spika wa bunge, Anna Makinda.

Amegusia mambo mengi yakiwemo, mfumo wa elimu, mfuko wa JK, tatizo la maji (na madhara yake kwa wanawake) nk.

Amelaani upotoshaji unaofanywa na Spika wa bunge, ufutaji wa hoja bungeni bila kufuata kanuni za bunge, na upendeleo bungeni.

Amesisitiza kwamba wabunge wa CHADEMA, awataudhuria kwenye Kamati ya maadili ya bunge kama ilivyoelezwa na Spika, mpaka pale rufaa zao 10 zilizofikishwa kwenye kamati hiyo zitakapo patiwa ufumbuzi.

Dk Slaa amedai kwamba hatua itakayofuata ni kupeleka hoja hizo kwenye mahakama ya Wananchi.

Msikilize......

No comments:

Post a Comment