Monday 25 February 2013

MDAHALO WA WA PILI WA WAGOMBEA URAIS KENYA

Ni wiki moja kabla ya uchaguzi mkuu wa Kenya ambapo wagombea urais watakutanishwa kwa mara ya pili ili kujinadi kwa kujibu hoja za wananchi.

Uchaguzi mkuu utafanyika jumatatu ya 04 March 2013. Mdahalo huu utahusisha maswala ya Uchumi, Ardhi na Mali asili na Sera za mambo ya nje.

Washiriki wote wa mdahalo wa kwanza uliofanyika 11 Feb 2013, wamethibitisha kushiriki isipokuwa mgombea wa Jubilee Alliance, Uhuru Kenyatta. Swala la ardhi linamuhusu Bw Kenyatta kutokana na kumiliki kiasi kikubwa cha ardhi, hivyo uenda ikachangia kutoshiriki kwake.

Mdhahalo huo utaanza saa 19:30 kwa saa za Afrika ya mashariki, na utarushwa hewani kupitia vyombo mbali mbali vikiwemo mitandao ya www.nation.co.ke , www.ntv.co.ke , ..

No comments:

Post a Comment