Sunday 13 January 2013

MECHI ZA 13 JANUARY 2013 - LIGI KUU YA UINGEREZA

16:30 Manchester Utd  2 - 1 Liverpool
19:00 Arsenal 0 - 2 Manchester City

NB: Saa za Afrika Mashariki

Wababe ni wababe  vibonde ni vibonde!

Arsenal ilipigwa red card  dk ya 10, Man City wakatumia mwanya huo na kufanikiwa kupata bao la kwanza dk ya 21 kupitia Milner, na dk 11 baadae Man City ikaongeza bao la pili kupitia Dzeko. Arsenal walishindwa kufurukuta hata baada ya Man City kupewa redcard dk 25 kabla ya kipenga cha mwisho.

Van Parsie aliipatia Man U bao la kuongoza dk ya 19 ya kipindi cha kwanza. Vidic naye akaongeza bao la pili dk ya 9 ya kipindi cha pili, hatimaye dk tatu baadae Sturidge akaipatia Liverpool bao la kufutia machozi.  

Msimamo wa top ten ulivyo (point mabanoni): 1.Man Utd (55), 2.Man City (48), 3.Chelsea(41), 4.Tottenham(40), 5.Everton(37), 6.Arsenal(34), 7.West Brom(33), 8.Liverpool(31), 9.Swansea(30), 10.Stoke(29)

Arsenal na Chelsea zina mechi moja kufikisha jumla ya mechi 22 zilizochezwa na timu nyingine. 

---------------------------------------------------------------------------------------------------
Man Utd inaongoza ligi ikiwa na ziada ya point 7 mbele ya Man City yenye point 45. Arsenal ipo nafasi ya 6 ikiwa na point 34, wakati Liverpool ipo nafasi ya 8 ikiwa na point 31.

No comments:

Post a Comment