Saturday 20 October 2012

SHEIKH FARID APATIKANA, AELEZEA YALIYOMSIBU

Baada ya kutoweka tangu tarehe siku ya Jumanne (16 October 2012), hatimaye kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho, Sheikh Farid amepatikana Ijumaa (19 October 2012) jioni.

Akielezezea yaliyomsibu kwenye mahojiano, Sheikh Farid alisema kwamba alichukuliwa na watu walio jitambulisha kama askari polisi kwa kuonyesha vitambulisho vyao, baadhi yao walikuwa na silaha. Walimchukua kwenye gari na kumfunga kitambaa usoni kisha kumpeleka kwenye nyumba asiyoitambua.

Amedai askari hao wenye lafudhi za Bara na wengine Visiwani, walitaka kujua kuhusu harakati zake zikiwemo safari zake za nje zikiwemo za Uarabuni na mahusiano yake na baadhi ya viongozi wa serikali. Pia askari hao walichukua simu yake na kumuhoji mengi kuhusu namba na message zilizopo kwenye simu yake. Watu hao walimrudisha eneo walilomchukua wakamfungua pingu na kitambaa cha usoni kisha wakamuachia huru.

Alisema watu hao waliomchukua kwa gari walikuwa wanne, akiwepo dereva na mwingine aliyekaa mbele ambaye alijitambulisha kwake, na nyuma ya gari walikuwepo watu wawili waliovaa kofia zilizofunika nyuso zao.

 
Ustaadhi Farid (mwenye kofia na kanzu) na wanawe baada ya kurudi nyumbani.

Kuhusu msimamo wake, Sheihk Farid amesisitiza kwamba wataendelea kuitetea Zanzibar mpaka iwe huru kama ilivyokuwa mwaka 1963.

Kumsikiliza zaidi twanga link http://www.mzalendo.net/habari/breaking-news-sauti-ya-ust-farid-na-salma-said

No comments:

Post a Comment