Friday, 19 October 2012

KUPOTEA KWA SHEIKH FARID, FUJO ZANZIBAR NA JUMUIYA YA UAMSHO

Huko Zanzibar, Mkoa wa Mjini Magharibi, fujo zilizuka siku ya Jumatano (17 Oct 2012), ambapo askari mmoja aliuwawa kwa kukatwa mapanga.

Fujo hizo zilizuka baada ya kutoweka kwa Sheikh Farid, ambaye ni kiongozi wa Jumuiya ya UAMSHO -  http://www.youtube.com/watch?v=ZvO712F2OW8&feature=youtu.be

Taarifa za polisi zimeeleza kwamba Sheikh Farid alionekana kwa mara ya mwisho siku ya Jumanne (16 Oct 2012) katika eneo la Mazizini akiongea na watu aliowaita, waliokuwa kwenye gari aina ya Noah.

Taarifa hiyo za polisi zimedai kwamba, wakati taarifa za kupotea kwa Sheikh Farid tayari zimepelekwa polisi Jumatano (17 Oct 2012), wafuasi wa Jumuia ya Uamsho walijikusanya katika msikiti wa Mbuyuni na kuazisha fujo zilizosambaa maeneo mengine, na kusababisha kifo cha askari polisi mmoja na uaribifu wa mali ikiwemo kuchoma ofisi za CCM, kuvunjwa kwa duka la pombe na kuiba mali zilizokuwepo ndani.

Uamsho ni nini?
'Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu' (JUMIKI) ni NG'O iliyoanzishwa na kusajiliwa kisheria mwaka 2001 na makao yake makuu ni Zanzibar.

Baadhi ya madhumuni ya Uamsho ni kuleta Mapenzi, Umoja na Maendeleo miongoni mwa waumini wa Kiislamu, pia kusaidia kutatua matatizo katika kijamii. Malengo yake yanafanikishwa kwa njia za miadhara, semina, nk.

No comments:

Post a Comment