Thursday 19 July 2012

WABUNGE WAMGOMEA SPIKA, WATOKA NJE KUDAI KIKAO KIHAIRISHWE ILI KUOMBOLEZO AJALI YA MELI ZANZIBAR

Baadhi ya maamuzi yasiyojali maslahi ya Wananchi na msimamo mgumu wa Spika wa bunge, imezaa matunda baada ya wabunge wa chama tawala na upinzani kwa pamoja kutoka nje ya kikao.

Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid alimuomba spika wa bunge kuhahirisha kikao cha 19 July 2012 mpaka 20 July 2012 (kesho), kama sehemu ya maombolezo kufuatia ajali ya meli ya MV Skagit iliyozama 18 July 2012 karibia na eneo la Chumbe, Zanzibar.

Lakini Spika, Anne Makinda alikataa ombi hilo kwa moyo mkunjufu, ndipo wabunge walipoamua kutoka ya kikao kama ishara ya kupinga msimamo wa Spika.

Wabunge wanawakilisha wananchi bungeni, Wabunge wanaongea kwa niaba ya wananchi. Wananchi  wamepatwa na msiba, Spika hakuona hilo, What a shame......!


No comments:

Post a Comment