Sunday 17 June 2012

MWANAUME AOTA MATITI BAADA YA KUTUMIA DAWA YA ARV's

Khamis Tanga, mwenye umri wa miaka 46, ameota matiti baada ya kutumia dawa ya kupunguza makali ya UKIMWI, ARV's.
Khamisi (pichani) ambaye ni mkazi wa kijiji cha Magomeni Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani amedai alianza kuota matiti miaka mitatu iliyopita baada ya kuanza kutumia dawa hizo.

Alitoa maelezo hayo kwa Waandishi wa Habari za Ukimwi -AJAAT (Association of Journalists Against Aids in Tanzania), waliofika eneo hilo kufanya utafiti kuhusu utekelezaji wa Sheria ya Ukimwi.

Anadai ameangaika sehemu tofauti, hadi Hospitali ya Muhimbili bila mafanikio, hivyo anawaomba Watanzania, pia Mh. Rais Jakaya Kikwete, kumwezesha kuondokana na hali hiyo.

Hata hivyo mtaalamu wa magonjwa, Dk Dina Komakoma amedai kwamba madhara hayo ni mojawapo ya matokeo ya matumizi ya dawa hizo, madhara mengine ni kunenepa, kukonda nk

Twanga link kujua zaidi http://bashir-nkoromo.blogspot.co.uk/

No comments:

Post a Comment