Sunday 17 June 2012

MECHI ZA 17 JUNE 2012 - KOMBE LA MATAIFA YA AFRICA (AFCON)

16:00 Zimbabwe 1-0 Burundi
16:00 Mozambique 9-8 Tanzania
17:30 Congo 3-0 Seycheles
18:00 Benin 1-1 Ethiopia
18:30 Togo 1-0 Kenya

NB: Saa za Afrika Mashariki

Ohhh, Kweli ngombe wa Maskini......! Au rizki aikuwa yetu!

Taifa Stars (Tanzania) imetolewa kwenye michezo ya Africa Cup of Nations. 

Taifa Stars ilipigwa na butwaa katika dk ya 8 ya kipindi cha kwanza, Mozambique ( a.ka Msumbiji )ilipofanikiwa kupata goli lililodumu mpaka mapumziko.

Kipindi cha pili Taifa Stas walifanikiwa kupata bao kusawazisha na kufanya dk 90 kumalizika timu zikiwa 1-1.

Matuta (penalty) yakapigwa Mozambique wakapata 8, Tanzania 7, na kufanya mechi kumalizika kwa Mozambique kushinda kwa jumla ya magoli 9-8.

Timu zilizo songa mbele: Zimbabwe, Mozambique, Congo(DR), Benin, na Togo

Timu Nyingine zilizofanikiwa Jumamosi ni: Malawi, Uganda, Cameroon, Nigeria, Sierra Leone, Liberia, na Cape Verde. Algeria ilifanikiwa Ijumaa

Imebakia timu moja ambaye ni mshindi kati ya Egypt v Central Africa Rep( CAR), mechi hii itachezwa tarehe 24 June 2012. 


----------------------------------------------------------------------------------------------------------
Taifa Stars (Tanzania), lazima ishinde ili iweze kusonga mbele kwenye mashindano ya kuwania kucheza final za Africa Cup of Nations (Afcon)2013.

Katika mzunguko wa kwanza, Burundi ilishinda 2-0 dhidi ya Zimbabwe, Congo nayo ilishinda 4-0 dhidi ya Seycheles, Mozambique na Tanzania zilitoka sare, Benin ilitoka sare dhidi ya Ethiopia,Kenya iliifunga Togo 2-1.

Kwa mechi za UEFA Euro 2012 angalia habari iliyotangulia hapo chini.

No comments:

Post a Comment