
Amir Khan na Lamont Peterson
Wababe hawa wawili walitarajiwa kukutana tarehe 19 May 2012, ikiwa ni marudiano kufuatia utata uliojitokeza kwenye pambano la kwanza lililofanyika December 2011.
Katika pambano la kwanza lilofanyika Washington DC, Peterson alishinda kwa Split Decision (113-112, 113-112, 110-115) na kunyakua mikanda ya WBA na IBF iliyokuwa inashikiliwa na Amir Khan.
Kufuatia matokeo hayo ndoto za Amir za kunyakua mikanda mingine ya WBO na WBC na kutaka kupambana na Mayweather zikayeyuka.
Hata hivyo kambi ya Khan ilifichua kasoro nyingi na kuziwasilisha WBA, ambapo iliamuliwa mpambano huo urudiwe 19 May.
Pambano lililokuwa lifanyike Las Vegas, May 19 limefutwa baada ya Peterson kubainika kutumia madawa ( synthetic testosterone) kinyume na taratibu, ambayo pia amekiri kuyatumia kwenye pambano la kwanza.
Amir anatafuta mpinzani mwingine atakaye pambana naye June 30.
No comments:
Post a Comment