Thursday 20 October 2011

KENYA NA 'OPERATION LINDA NCHI'

Walicho kianzisha Al Shabaab, uenda ilikuwa ni kujichimbia kaburi!

Jeshi la Kenya linaendelea na 'Operation Linda Nchi', kufuatia vitendo vya utekaji vinavyodaiwa kufanywa na Al Shabaab. Nia ikiwa ni kulinda uchumi na mipaka ya nchi, kwa kushirikiana na serikali ya Somalia.

Hadi sasa wameshakufa askari 73 wa al Shabaab, na 5 wa jeshi la Kenya. Harakati hizo zimewezesha kuchukua miji ya Dhobley na Tabda na harakati zinaelekea miji ya  Afmadow , Beles Qooqani na hatimaye Kisimayu.


Harakati hizi zitahathiri vipi uchumi, usalama na hali ya maisha kwa ujumla kwenye nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki? Je harakati hizi zitafanikiwa kuteketeza kundi la Al Shabaab ama litasambaa zaidi? Je uchumi wa Kenya utaathirika vipi kama vita vitachukua muda mrefu zaidi? Na nini itakuwa matoke ya harakati hizi?

twanga hapa for more- http://www.nation.co.ke/News/Jets+hit+al+Shabaab+as+rain+delays+march+/-/1056/1258352/-/item/0/-/b23rqsz/-/index.html

No comments:

Post a Comment