Saturday, 7 April 2012

RIP STEVEN KANUMBA


Ni vigumu kuamini, lakini ndio mipango ya mungu!

Muigizaji maarufu nchini Tanzania, Steven Kanumba a.k.a 'The Great'  (pichani) hatunaye tena.

Sababu za kifo chake zinatokana na kuanguka nyumbani kwake Vatican Sinza, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo ambapo aliangukia kisogo, na juhudi za kuokoa maisha yake azikufanikiwa.

Inadaiwa Steven Kanumba alianguka baada ya kusukumwa na mpenzi wake baada ya kuzuka mzozo kati yao. Mpenzi huyo wa Kanumba aliyetajwa kwa jina Lulu pia ni maarufu kwenye mambo ya uigizaji nchini.

Steven Kanumba alizaliwa 08 January 1984.

Mungu ailaze roho ya marehemu Steven Kanumba mahali pema peponi.

No comments:

Post a Comment