Rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika inadhaniwa kuwa amefariki dunia.
Rais huyo mwenye umri wa miaka 78 aliugua ghafla jana (05 April 2012) na kulazwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) hospitalini mjini Lilongwe, na inasadikika kuwa baadae alipelekwa nchini Afrika ya Kusini kwa matibabu zaidi.
Rais Mutharika aliingia madarakani mwaka 2004 kupitia chama cha UDF (United Democratic Front), lakini baadae akajitenga na kuanzisha chama cha DPP (Democratic Progressive Party).
Kikatiba makamu wa rais anatakiwa kurithi madaraka iwapo rais aliyekuwa madarakani amefariki ama kushindwa kufanya kazi kwa sababu za kiafya.
Kulikuwa na kuelewana kati ya aliyekuwa makamu wa rais, Joyce Banda na rais Bingu wa Mutharika. Na kwenye mabadiliko ya baraza la mawaziri ya 08 September 2011 nafasi hiyo iliachwa wazi.
Badala yake Chama cha DPP kilimteua Peter Mutharika ambaye ni kaka wa rais Bingu wa Mutharika kuwa mgombea urais wa uchaguzi ujao wa 2014.
Lakini inasemekana kikatiba Joyce Banda bado ni makamu wa rais na ndiye mwenye wajibu wa kurithi nafasi ya urais kwa muda uliobaki mpaka uchaguzi ujao.
Nani atarithi urais, Joyce Banda ama Peter Mutharika? Au ndio mwanzo wa migogoro wa kisiasa nchi Malawi?
No comments:
Post a Comment