22:00 Arsenal 1-2 Wigan
NB: Saa za Afrika Mashariki
Baada ya Arsenal kuanza kwa kasi ya ajabu, lakini kinyume chake ni Wigan walio pata mabao mawili baada ya counter attack ya nguvu dk ya 6 na dk 8!
Dakika ya 21 Vermaelen akaipatia Arsenal bao pekee lililodumu mpaka dakika ya mwisho. Huu ni mwanya kwa Tottenham na Newcastle kuisogelea Arsenal.
Arsenal imebakiza mechi 4, na Jumamosi inacheza na Chelsea, kazi ipo!
Kwa matokea haya Wigan imefikisha point 34 na kupanda nafasi ya 18.
-----------------------------------------------------------------------------------------------
Katika mechi iliyopita Wigan walitoa kichapo cha 1-0 kwa Man Utd! Arsenal wakae mkao.
Arsenal inazo point 64 kwenye nafasi ya 3, ushindi ni lazima ili kulinda nafasi ya 3 sababu Tottenham (59), Newcastle (59) na Chelsea (57) zitaingia kwenye msafara wa kugombania nafasi ya 3.
Wigan ipo nafasi ya 17 na point 31 ushindi ni muhimu ili kujiondoa kwenye balaa la kushuka daraja.
Kesho: Nusu fainali UEFA ligi ya mabingwa - Bayern Munich v Real Madrid
No comments:
Post a Comment