20:00 Tottenham 1-5 Chelsea
NB: Saa za Afrika Mashariki
Mmmm! Kwa mtindo huu Tottenham hawastahili hata kushiriki kombe la mabingwa wa Ulaya (UEFA) msimu ujao. Pamoja na kwamba bao la pili Chelsea wamebebwa na mwamuzi wa mchezo, ni kama safu ya ulinzi ya Tottenham ilikuwa likizo.
Ushindi wa Chelsea ni ujumbe mzito kwa Liverpool kwamba fainali itakuwa ni patashika, aka Chelsea tayari ni mabingwa wa kombe la FA.
Kwa uchovu wa leo, Chelsea watasikilizia muziki laini watakapocheza dhidi ya Barcelona jumatano kwenye kombe la Mabingwa wa Ulaya (UEFA).
Swali- Fainali ya Kombe la FA ni lini?
Jibu- Ni Jumamosi, tarehe 5 May 2012
---------------------------------------------------------------------------------------------------
Mshindi wa mechi hii atapata ticket ya kucheza fainali dhidi ya Liverpool iliyoshinda dhidi ya Everton. Ni Tottenham ama Chelsea?
No comments:
Post a Comment