Saturday, 14 April 2012

MECHI ZA 14 APRIL 2012 - KOMBE LA FA UINGEREZA

14:30 Liverpool 2-1 Everton

NB: Saa za Afrika Mashariki

Haya hayaa, kumekucha Bwawani (Liverpool)! 

Neema yawashukia, waingia fainali ya kombe la FA. Everton walipata bao la kuongoza dakika ya 24 ya kipindi cha kwanza, Luis Suarez akasawazisha dakika ya 62. Katika dakika ya 86 Andy Carol akapachika bao la pili na kuipatia Liverpool ticket ya kucheza fainali.

Liverpool itacheza fainali na mshidi wa mechi ya kesho kati ya Tottenham na Chelsea. Tusiandikie mate!

--------------------------------------------------------------------------------------------------
Liverpool vibonde wa ligi kuu msimu huu, wamechukua kombe la Carling, na sasa wanatafuta kombe la FA, watafanikiwa kuwapiga Everton?

Kesho: Tottenham v Chelsea

Kwa mechi za Ligi kuu angalia hapo chini

No comments:

Post a Comment