Monday 2 April 2012

UCHAGUZI ARUMERU MASHARIKI - CHADEMA YASHINDA UBUNGE

Haya hayaaa  'Mwenye masikio ...................!

CHADEMA imeibua ushindi MNONO kwenye kinyang'anyiro cha kugombea kiti cha ubunge jimbo la Arumeru Mashariki, a.k.a Joshua Nassari ni mbunge kwa sasa!

                                              Joshua Nassari

Matokeo ya wagombea na kura zao ni kama ifuatavyo:-

Joshua Nassari (CHADEMA) ----32,972
Sioi Sumari (CCM) ---- 26,757
Abdalah Mazengo (AFB) ----139
Mohamed Mohamed (DP) ----77
Khamis Kihemu (NRA) ---- 35
K Moyo  (SAU) ----22
A Chipata (TLP) ---- 18
C Msuya (UPDP)---- 18

Walio jiandikisha kupiga kura walikuwa 120,000.Waliojitokeza kupiga kura ni 60,699  ambapo kura halali zilikuwa 60,038, na kura 661 ziliharibika.

Akiongea baada ya kutangazwa rasmi, Mh. Mbunge mteule Joshua Nassari ameliomba jeshi la polisi kuwaachia huru wananchi waliosekwa ndani baada ya kushangilia ushindi wake isivyo rasmi hapo jana, ili washerekee ushindi la sivyo naye yupo tayari kujiunga nao mahabusu.

Pia Mh.Mbunge mteule, Joshua Nassari amehahidi kufuatilia maswala ya ardi, maji, elimu, miundo mbinu na afya. Na amehahidi kufuatilia ahadi za uchimbaji visima alizoahidiwa na Ndesamburo, na kufuatilia uanzishaji wa mfuko wa wajane na yatima.

Hii ni aibu kubwa kwa CCM, kwani campaign zao zilihusisha viongozi wakubwa akiwemo rais mstaafu W.Mkapa, waziri mkuu mstaafu E.Lowasa na viongozi wengine waliojitokeza katika juhudi za kunusuru kiti hicho.

Tusiandikie mate, pata uondo mwenyeweee........


No comments:

Post a Comment