Msimu mpya wa Formula 1 na mambo mapya, ushindi wa kwanza wanyakuliwa na McLaren.
Katika race za kwanza zilizofanyika nchini Australia, Jenson Button aliyeanza kwenye nafasi ya pili amemaliza race hizo katika nafasi ya kwanza , naye Lewis Hamilton wa McLaren aliyeanza katika nafasi ya kwanza amejikuta akimaliza katika nafasi ya 3.
Mshindi wa msimu uliopita S.Vetel wa Redbull aliyeanza katika nafasi ya 6 amemaliza katika nafasi ya pili. Mark Webber aliyeanza nafasi ya 5 amemaliza katika nafasi ya 4.
Kwa upande wa Ferrari, Alonso alianza katika nafasi ya 12 alimaliza katika nafasi ya 5, huku mwenzake F.Massa aliyeanza katika nafasi ya 16 ameshindwa kumaliza race hizo.
M.Schumacher wa Mercedes GP alishindwa kumaliza race hizo ingawa alianza katika nafasi ya 4, mwenzake Rosberg alijikuta akirudi nyuma na kumaliza kwenye nafasi ya 12 ingawa alianza kwenye nafasi ya 7.
McLaren, Mercedes wanayo nafasi ya kufanya vizuri msimu huu, Ferrari bado awaeleweki na uenda ushindani bado utatolewa na Redbull.
Race zinazofuata : Malaysian Grand Prix, 25 March 2012
No comments:
Post a Comment